Thursday, August 2, 2012

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA NA CHETI- 2011/2012

Majina ya waliochaguliwa kujiunga na ualimu ngazi ya cheti BOFYA HAPA

Majina ya waliochaguliwa kujiunga na ualimu ngazi ya stashahada BOFYA HAPA

MAELEZO MUHIMU

Waombaji waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu katika mwaka wa masomo wa 2011/2012 wanatakiwa kuripoti katika vyuo walivyopangiwa tarehe 12/08/2012. Kwa wale watakaochelewa kupata barua za maelezo(joining instruction) kutoka vyuoni wanatakiwa kuripoti vyuoni katika tarehe iliyopangwa bila kukosa.
Wanafunzi wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo.
1: Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania Kidato cha Nne na Sita kulingana na kozi husika.
2: Ada kwa mwaka ni shilingi 200000/= (Mhula wa kwanza shilingi 100000/= na mhula wa pili shilingi 100000/=)
3: Sare ya chuo kulingana na maelezo ya chuo husika.
4: Fedha kwa matumizi binafsi.
Aidha kila mkuu wa chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SI vinginevyo.

0 Maoni:

Post a Comment