Sunday, June 17, 2012

WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE NA SITA NA KUCHAGULIWA KUFANYA USAILI KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI


Jeshi la Polisi (T) limetoa orodha ya majina ya vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2011 na waliomaliza kidato cha sita mwaka 2012 ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Usaili utafanywa katika kanda tisa ambapo kanda, vituo na tarehe za usaili zimeoneshwa.

Muhimu:

(i)         Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe na uhakika na amejiridhisha mwenyewe kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili. 

(ii)        Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika. 

(iii)      Mwombaji aje na barua za wadhamini wawili wanaomfahamu vizuri zikielezea uhusiano baina yao na mwombaji pamoja na anuani kamili za wadhamini hao na namba zao za simu zinazotumika kikamilifu. 

(iv)       Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia yeye mwenyewe gharama za usafiri hadi kwenye kituo cha usaili na kurudi kwao baada ya usaili, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

T. M. Andengenye -SACP
Kny: Inspekta Jenerali wa Polisi 1) Tangazo kamili la usaili, kanda, vituo na tarehe za usaili BOFYA HAPA

2) Majina ya waliomaliza kidato cha nne na sita waliochaguliwa kufanya usaili kujiunga na jeshi la polisi SOMA HAPA
0 Maoni:

Post a Comment