Saturday, February 28, 2015

MAFURIKO YAWAUA WATU 14 MADAGASCARWatu 14 wameuawa kwenye mafuriko nchini Madagascar ambapo pia wengine 20,000 wamelazimika kuhama makwao.

Mafuriko hayo yaliukumba mji mkuu Antananarivo na maeneo yaliyo karibu.Utawala unasema kuwa mvua nyingi siku zijazo huenda ikasababisha madhara zaidi.

Mvua kubwa imenyesha nchini humo kwa takriban wiki mbili.Mwezi uliopita kimbunga Chedza kiliwaua watu 80 nchini Madagascar.

Chanzo: BBC

MATOKEO YA LIGI KUU UINGEREZA(EPL) JUMAMOSI FEBRUARI 28.


KAPTENI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA

 Kapteni John Komba akitumbuiza siku ya maadhimisho ya miaka 38 tangu kuzaliwa CCM.


Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki dunia leo alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .

Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto kumi na moja.

Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni leo akiwa mahututi

"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," amesema Dk Ishan

Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.

RATIBA YA LIGI KUU UINGEREZA(EPL) LEO JUMAMOSI FEBRUARI 28.

Mechi zote ni saa 12.00 jioni, isipokuwa mechi kati ya West Ham United na Crystal Palace ambayo ni saa 9.45.